Wanachama
watatu wa Chadema wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na
kuunganishwa na wenzake 28 wanaokabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko isivyo
halali.
Washtakiwa hao
wamepandishwa kizimbani leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa
wakiwa na majeraha miguuni huku sehemu ya mapaja wakiwa wamefungwa bandeji
Wakili wa
Serikali, Patrick Mwita amewasomea hati ya mashtaka inayowakabili washtakiwa
hao watatu ambao ni Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi.
Washtakiwa
hao, Machi 8, 2018 wataunganishwa na wenzao 28 ambao ni Thabita Mkude, Haji
Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mrombo, Abdallah Hamis,
Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edna Kimoro
Wengine ni
Jonathan Lema, Salha Ngondo, Ramadhan Mombo, Godwin Mwakasungura, Hassan
Kibweda, Omary Hamad, Fatima Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa, Dickson
Kerefu, Raphael Mwaipopo, Athuman Mkawa, Mussa Kusigila, OMARY Danga, Jackson
Masilingi, Asha Kileta na Ally Rajabu.
Kwa pamoja
wanadaiwa Februari 16, 2018 katika eneo la Kinondoni Mkwajuni lililopo
katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa
halali kinyume cha sheria.
Ilidaiwa kuwa
mkusanyiko huo ulikuwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha
taharuki kwa wananchi
Washtakiwa
wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana kwa kila mshtakiwa kuwa na
mdhamini mmoja ambaye alisaini ahadi ya Sh1.5 milioni na kutakiwa kutotoka nje
ya Jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Upelelezi bado
haujakamilika.
Baada ya
kuachiwa kwa washtakiwa hao watatu ndugu zao waliwakumbatia na kuangua vilio
WATU WATATU CHADEMA WAPANDISHWA MAHAKAMANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment