Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wanachama wa Chadema baada ya upande wa
mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yao pasipo kuacha shaka.
Washtakiwa
walioachiwa huru na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba leo Jumatano Februari 28,
2018 ni; Sunday Urio, Kizito Damia, Joseph Samky, Chrisant Clemence,
Wilfred Ngowi, Karim Ally na Kinyaiya Siriri.
Kwa pamoja
walikuwa wanakabiliwa na tuhuma za kufanya fujo na kuwazuia askari polisi
kufanya kazi yao
Akisoma hukumu
hiyo leo, hakimu Simba amesema wajibu wa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha
shaka ni wa upande wa mashtaka na siyo upande wa utetezi .
Akiendelea
kusoma hukumu hiyo amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu wa upande
wa mashtaka, hakuna sehemu walisema, waliwaona washtakiwa wakirusha mawe kwa
polisi na kuwazua wasifanye kazi yao.
Katika kesi
hiyo washtakiwa walionekana na kesi ya kujibu na katika utetezi wao karibia
wote ulikuwa unafanana kuwa hawakuwepo eneo la tukio na wala hawakutenda kosa
waliloshtakiwa nalo.
Hivyo
aliwaachia huru washtakiwa hao.
Katika kesi hiyo wanadaiwa, Januari 26,
mwaka 2015 huko Ubungo eneo la Riverside, kwa makusudi walifanya fujo kwa
kuwarushia mawe askari polisi wa kutunza amani ili washindwe kufanya kazi yao.
WANACHAMA WA CHADEMA WAACHIWA HURU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment