Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa
Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ally Samaje,
imeshindwa kuendelea baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa hawajaanda maelezo
ya awali.
Kwa mara ya kwanza, Samaje alifikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Februari 9, 2018 kujibu mashtaka mawili ya matumizi mabaya
ya madaraka.
Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai amedai leo Februari 28,
2018 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa
ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini bado hawajaanda
“Shauri hili lilikuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja
za awali, lakini bado hatujaziandaa, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili
ya kuziandaa na kumsomea” alidai Swai
Baada ya maelezo hayo, hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo
hadi Machi 28, 2018 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na
mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
Katika kesi ya msingi, Swai amedai kuwa mshtakiwa huyo
alitenda makosa hayo kati ya Aprili 9 na Juni 21, 2013 Makao Makuu ya Wizara ya
Nishati na Madini iliyopo wilaya ya Ilala.
Hata hivyo, Samaje ambaye anatetewa na wakili Jema Bilegea,
yupo nje kwa dhamana baada ya kusaini ahadi ya Sh 50milioni na hatakiwi
kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.
Aliyekuwa kaimu kamishna wa madini asomewa maelezo ya awali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment