WAKALA wa Chakula, Dawa na Vipodozi
Zanzibar, imezuia kuingiza nchini tani 150 za mchele aina ya red rose wenye
thamani ya zaidi ya Sh. milioni 180 katika Bandari ya Malindi Zanzibar.
Mchele huo uliotoka nchini Pakistani
ambao ni mali ya GAGO Store, uliingizwa nchini Februari 13, mwaka
huu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara na kugundulika haufai kwa
matumizi ya binadamu
|
Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Udhibiti, Usalama, Chakula katika Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi, Dk.
Khamis Ali Omar, alisema mchele huo pia haukidhi vigezo vya vifungashio na
maandishi na kuweka taarifa zisizo sahihi kwa kuandikwa mchele grade namba
moja wakati si kweli
|
Aidha, alisema mchele huo
ulionyesha ulikusudiwa kwa soko la Mauritius badala ya Zanzibar jambo ambalo
ni kinyume na utaratibu za uagizwaji wa bidhaa za chakula nchini
|
Alisema hatua zitakazochukuliwa ni
mwenye mali kuurudisha mchele huo ulikotoka na akishindwa hatua zitakazo
chukuliwa ni kuteketeza mchele huo, ili usiweze kuathiri jamii.
|
|
Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa
athari zinazotokana na chakula, Aisha Suleiman Mbandakazi, alisema athari
zinazotokana na chakula kisichofaa kwa matumizi ya mwanadamu ikiwamo mchele
ni pamoja na matatizo ya akili, ukungu unaozalisha sumu kuvu
inayosababisha matatizo ya ini pamoja na kizazi.
|
|
|
No comments:
Post a Comment