DC CHONGOLO ATANGAZA MSAKO WA BOMA KWA BOMA KUWASAKA WALIOKEKETWA


MKUU wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, amesema wanatarajia kuanza ukaguzi wa boma kwa boma kuwabaini   watoto waliokeketwa na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi
Alisema hayo katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga mimba na ndoa za utotoni kwa ngazi ya wilaya iliyoandaliwa na Mratibu wa Miradi wa Kitumbeine, ulio chini ya Shirika la World Vision Tanzania (WVT

Mradi huo unajihusisha na masuala ya afya, elimu, utetezi, kilimo, mifugo na uchumi.
Hata hivyo, alisema, hawezi kutaja siku ya kuanza ukaguzi huo utakaowashirikisha maafisa afya kwa kila boma.Alisema ukaguzi huo utahusisha pia watu waliowapa mimba watoto na kuwaoa
“Wapo wanaooa mimba, baadaye wanajipitisha kwa kutengeneza mazingira ya kuwapa mimba, hakutakuwa na     mswalia Mtume kwa jambo hili,” alisema.
“Nitaanza na hilo, wataalam wa afya watapita kufanya ukaguzi wa watoto, wakibainika wazazi wao watafikishwa mahakamani,” alisema

Alisema uamuzi wa kufanya ukaguzi umekuja baada ya kubaini kwamba hakuna watu wanaofikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya ukatili huo.


DC CHONGOLO ATANGAZA MSAKO WA BOMA KWA BOMA KUWASAKA WALIOKEKETWA DC CHONGOLO ATANGAZA MSAKO WA BOMA KWA BOMA KUWASAKA WALIOKEKETWA Reviewed by KUSAGANEWS on February 28, 2018 Rating: 5

No comments: