Serikali imepeleka
shilingi bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa
ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya na kuwasisitizia watendaji
kutobadilisha matumizi ya fedha hizo wazipatapo.
Hayo yalibainika wakati Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara ya kikazi
mkoani Mtwara na kusema fedha hizo zilitolewa na serikali ili kuimarisha
upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Waziri Mkuu amesema ujenzi huo
utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama
na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha
kuhifhadhia maiti.
"Serikali imeamua kuimarisha
sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma za afya karibu na makazi yao", amesema Waziri Mkuu.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka
wananchi hao kuendelea kuiunga mkono serikali yao ambayo imedhamiria
kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.
Pia Waziri Mkuu amesema serikali
inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka
masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.
Bilioni 1.92 zatolewa na serikali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment