Kamati ndogo ya Umoja wa
Mataifa kuhusu kuzuia vitendo vya utesaji na unyanyasaji 'SPT' imeamua kurejea
nchini Rwanda baada ya kusimamisha uchunguzi huo Oktoba 2017, ingawa tarehe ya
kurejea huko haijatangazwa mpaka hivi sasa.
Ziara hiyo iliamuliwa wakati wa
kikao cha SPT kilichofanyika mjini Geneva Uswisi ambapo kamati hiyo vilevile
imeamua kudurusu orodha ya mataifa ambayo hadi sasa yameshindwa kuunda chombo
cha kitaifa kinachochunguza uzuiaji katika kipindi cha miaka minne baada ya
kuudhinisha.
Kamati ndogo ya kuzuia utesaji-SPT
inauwezo kufanya ziara yoyote ya kushtukiza kwa eneo lolote ambapo haki za watu
zikiwa zinakiukwa katika nchi ambayo iliidhinisha itifaki ya mkataba wa kuzuia
utesaji.
Vituo hivyo vinaweza kuwa ni
magereza, vituo vya polisi, vituo vya kuwazulilia wahamiaji, vituo vya
kuwashikilia watoto, vifaa vya kudodosa, na hospitali za watu walio na ulemavu
wa akili.
UN KUFANYA UCHUNGUZI WA VITENDO VYA UTESAJI NA UNYANYASAJI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment