Serikali ya Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania imefanya mabadiliko na kuibadili kampuni ya
simu ya TTCL kuwa shirika la Umma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametangaza maamuz hayo leo alipokuwa akiongea
na waandishi wa habari na kusema kuwa mabadiliko hayo hayawezi kuathiri wateja
wa TTCL
"Sasa tunatoka kwenye TTCL
kampuni na kuwa shirika la Umma tunaamini saizi mtajipanga zaidi kwenye mambo
ya usalama na uimarishaji mambo ya uchumi. Pia napenda kuwajulisha Watanzania
kuwa mabadiliko haya hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali
ambazo zilikuwa zikitolewa na kampuni ya simu ya TTCL, huduma zote zilizokuwa
zikitolewa kuanzia kwenye simu za mkononi, data, enternet, TTCL Pesa zote
zitaendelea sasa kwa kiwango kikubwa zaidi" alisema Mbarawa
Mbali na hilo Mbarawa amewataka TTCL
sasa kufanya jitihada za kwenda kukusanya madeni yake kwa wananchi mbalimbali
ambao wanatumia huduma zao na kusema kuwa Serikali inatambua ina deni kwa TTCL
na kuwa wao watalipa na wako tayari kulipa ila wanapaswa kuanza kwenda kudai
fedha zao kwa wananchi mbalimbali na makampuni ambayo pia yanadaiwa na
TTCL.
SERIKALI YASEMA KWASASA TTCL NI SHIRIKA LA UMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment