Kubenea Wapo vijana wanaolaghai wapiga Kura

Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea amevitaka vikundi vinavyodaiwa kuwa vya CCM vinavyozunguka kuandikisha vitambulisho vya watu kuacha mara moja kabla hawajachukua hatua ambazo amezitaka zisilaumiwe.

Akizungumza leo na wanahabari, Kubenea amesema kwamba wamegundua wapo vijana ambao wamekuwa wakilizunguka jimbo la Kinondoni na kuwalaghai wapiga kura kwa kununua vitambulisho, kuchukua shahada pamoja na kununua vitambulisho hivyo ili kupunguza idadi za wapiga kura kwa makusudi.

Kubenea amesema kwamba endapo vikundi hivyo vitakaidi agizo hilo watashughulikiwa kama wahalifu kwani kitend wanachokifanya ni kitendo cha uhalifu.

"Mnyika alituambia jana kuwa wanaofanya hivyo ni vibaka kama vibaka wengine, hivyo wanapaswa kushughulikiwa.  Na sisi tunasema kwamba Tutaingiza vijana wetu mitaani ili washughulikiwe na lolote litakalotokea wasituulize." Kubenea

Pamoja na hayo kubenea amesema kwamba tayari wamekwishapeleka malalamiko yao katika vyombo husika.

Kubenea kwa sasa ndiye Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Salum Mwalimu wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Februari 17
Kubenea Wapo vijana wanaolaghai wapiga Kura Kubenea Wapo vijana wanaolaghai wapiga Kura Reviewed by KUSAGANEWS on February 01, 2018 Rating: 5

No comments: