Rais Dkt. Magufuli
leo Februari 1, 2018 amewabadilikia Waziri wa Katiba na Sheria, Prof.
Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju kuwa
wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo ya
msingi.
Magufuli amesema hayo alipokuwa
kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria na kusema yeye ameubwa kusema ukweli hivyo
ataendelea kuusema hata kama kuna watu unawaumiza
"Kinachoshangaza pamoja na
hatua nzuri ya Serikali kupeleka 'Legal Aid Act' ya mwaka 2017 na mapendekezo
mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini 'regulation' mpaka saizi
hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy
AG yupo jamani mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa kwa hiyo
wewe Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna 'Instrument' za kuweza kutoa
uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini
regulations mpaka leo miezi tisa imepita"
Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa
"Watu wapo wanakula tu
mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda
mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji
wake hawatoi haki kwa Watanzania, ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo
ndani ya Serikali lazima na mimi nijitathimini ninachaguaagaje hawa watu ambao
wanachelewesha chelewesha, hiyo ndiyo tathimini ambayo ninaanza kujifanyia
kuanzia leo" alisema Rais
Magufuli
Magufuli amshukia Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment