Naibu Waziri wa
Afya, Dkt. Ndugulile leo Februari 1, 2018 amefunguka na kusema Serikali
haijazuia wanafunzi wa kike kutoendelea na masomo baada ya kupata ujauzito bali
ilizuia mwanafunzi kurudi shule aliyokuwa akisoma awali kabla ya kupata
ujauzito.
Ndugulile amesema hayo leo Bungeni
wakati akijibu swali ambalo liliulizwa na Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA,
Halima Mdee ambaye alitaka kujua juu ya utekelezaji wa sera ya 're entry
policy' ambayo ilianzishwa katika kipindi cha awamu ya nne ya Serikali
kuwawezesha wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule baada ya kujifungua
kupata haki yao ya kimsingi ya kusoma.
Akijibu swali hilo Ndugulile alisema
kuwa "Ni kweli kulikuwa na maandalizi ya 're entry policy'
lakini utekelezaji wake sasa umepitwa na wakati kutokana na agizo lililotolewa
na Serikali kwamba mtoto ambaye amepata ujauzito hataruhusiwa kurudi katika
shule ambayo alikuwa anasoma lakini maagizo haya hayajazuia mtoto wa kike
ambaye amepata ujauzito kutoendelea na masomo hapo naomba tuelewane vizuri.
Serikali imezuia mtoto wa kike kurudi shule aliyokuwa akisoma ila haijazuia
mtoto wa kike kuendelea na masomo" alisema Ndugulile
Mbali na hilo Naibu Waziri huyo
amesema kuwa sasa Serikali inaangalia njia mbadala ambayo itawawezesha watoto
wa kike ambao wamepata ujauzito ili waweze kuendelea na masomo.
Baada ya kauli ya Naibu Waziri
aliibuka Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa.
Joyce Ndalichako na kuweka msimamo wa Serikali kuwa mwanafunzi ambaye
amepata ujauzito hawezi kurudi shule kama ambavyo Naibu Waziri wa Afya amesema.
Mwezi June 23, 2017 Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema serikali yake
haitoruhusu mwanafunzi aliyepata ujauzito kuendelea na masomo.
Tazama hapa jinsi ambavyo Mawaziri
walikuwa wakijibu swali la Mbunge Halima Mdee
HATUJAZUIA MTOTO WA KIKE ALIYEPATA UJAUZITO KUENDELEA NA MASOMO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment