Watu wasiojulikana na
CUF wamekishtaki CHADEMA kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi jimbo la Kinondoni kuwa
chama hicho kimekuwa kikiuka utaratibu wa kampeni na kuvunja kanuni na maadili
ya uchaguzi, jambo ambalo CHADEMA wamelipinga vikali na kudai ni hujuma.
Mkurungenzi wa Oganezesheni na
Mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Benson Kigaira amesema
kuwa matatizo ambayo tayari yamejitokeza kwenye chaguzi mbalimbali toka
Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani yameanza kujitokeza tena kwenye
jimbo la Kinondoni hivyo wameamua kusema mapema ili wahusika wanaohusika na
uchaguzi waweze kuona.
"Tunadhani Kinondoni
inakwenda kuwa na shida kuliko wakati mwingine wowote kwa sababu hiyo tukaona
tuzungumze mapema ili kuondoa mambo ambayo yanaweza kupelekea shida kwenye
uchaguzi. Nimeona niletea haya mambo muone kwani hawa watu tayari wana nia
mbaya kuna barua mbili za malalamiko ya maadili dhidi ya CHADEMA, barua ya
kwanza ni kichekesho zaidi kwani maadili wanatakiwa kushtakiana au kutuhumiana
ni washiriki wa uchaguzi haiwezekani polisi itatuhumu chama cha siasa dhidi ya
maadili na polisi huwezi kuituhumu kwa maadili. Sasa lalamiko la kwanza
Mkurugenzi anasema amepokea taarifa kwa mtu asiejulikana kwamba CHADEMA
kinavunja kanuni za maadili"
Kigaira aliendelea kusema kuwa "Mkurugenzi
anaeleza anasema tarehe 28 Januari mlifanya kampeni nyumba kwa nyumba na
maandamano Kigogo kuanzia Mbuyuni mpaka Ronda Bar na aidha anasema maandamano
yalifanyika nje ya muda uliopangwa. Kwa barua hii anataka kusema kuwa huyo mtu
asiyejulikana maana anasema amepata taarifa lakini sheria inataka kuwe na
mlalamikaji, Mkurugenzi anaandaa malalamiko ambayo sio ya kweli ili atoe hukumu
yake aliyoiandaa, anasema tar 28/1/2018 tulipaswa kuwa Ndugumbi Kagera
Mikoroshini na si Kigogo. Sisi tulikuwa Kigogo kama ratiba inavyoonyesha ambayo
pia yeye anayo"
CUF WAISHTAKI CHADEMA KWA MKURUGENZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment