Serikali ya Tanzania
kupitia Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amesema hawaitaji tena
kuendelea kupata aibu katika kuendesha kesi ndani ya Mahakama zilipo nchini
kwani kwa sasa watatumia mfumo mpya wa tehama kuhifadhi jalada mbalimbali.
Profesa Ibrahimu Juma ameeleza hayo
leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa
mwaka mpya wa kimahakama yaliyofanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi
akiwa Rais John Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi.
"Mahakama imejiwekea malengo ya
kuongeza uwazi na ufanisi katika masuala ya utawala na uendeshaji wa mashauri
na tehama tumeona ndio jibu sahihi kwa Mahakama karne ya 21 inayolenga
kuwa na uwazi pamoja na ufanisi...
Mahakama hatuhitaji tena aibu ambazo
zimezoeleka za jalada zilizopotea au halionekani, hatuhitaji hadithi ya
jalada linahitaji kufutwa vumbi kwanza au stakabadhi ya malipo ya shughuli
haionekani, hatutaki kusikia mteja shauli lake liko wapi, kwa nani na ni lini
au lipo mbele ya Jaji yupi", alisema
Profesa Ibrahimu Juma.
Pamoja na hayo, Jaji Mkuu aliendelea
kwa kusema "tumepanga kufuta hayo yote ili kujenga historia
mpya katika msingi wa tehama, tumeadhimia na hatutaki kubaki nyumba na
tutaendelea na kasi ya mabadiliko ya kunufaika kutokana na mafanikio makubwa ya
tehama tumelenga kuyashuhudia na kunufaika na manufaa ya tehama kwenye eneo la
usimamizi wa fedha, ukosaji wa takwimu, mapato, usikilizaji wa mashauri".
Kwa upande mwingine, Profesa
Ibrahimu Juma amemkumbusha Rais Magufuli lengo la kusogeza huduma karibu na
wananchi kwa kuanzisha Mahakama zinazotembea ili kuweza kuwafikia popote
walipo.
SERIKALI HATUTAKI TENA KUPATA TABU KATIKA KUENDESHA KESI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment