Rais John Magufuli
amewapa pole Majaji kwa changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapo shughulikia
mashitaka yanayopelekwa na serikali na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kabla
ya mwezi Februari kuisha kwa madai ameshajifunza vya kutosha.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo
wakati alipohudhuria kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi
wa mwaka mpya wa kimahakama yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo yeye
binafsi ndio alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo akiongozana na viongozi
wengine wa serikali.
"Kwa kuadhimisha siku hii ya
sheria maana yake ni kwamba nchi yetu inatambua umuhimu wa sheria katika
kusimamia haki, kudumisha amani na kuleta maendeleo ya nchi. Maadhimisho haya
ya siku ya sheria ni muhimu kwa vile yanatoa fursa kwa vyombo vinavyohusika na
masuala ya sheria na utoaji haki", alisema
Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli alisema bado
kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG
(Mwanasheria Mkuu), na ndio maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto
kubwa Majaji.
"Najua mnapata shida sana
mnapo-dili na mashitaka yanayoletwa na serikali mnauona kabisa ushahidi upo
lakini watetezi hawajitokezi hadharani kuutetea. Mwaka jana nililalamika lakini
mwaka huu nitalishughulikia vizuri. Sitalalamika tena ninajua nitakavyofanya
kwa sababu nimeshajifunza vya kutosha na nimejua wapi kuna 'weakness' na wala huu
mwezi wa Februari hautoisha", alisisitiza
Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli
amewataka viongozi wengine wanaosimamia vyombo vya sheria kufuata mfano mzuri
aliyouanzisha Profesa Ibrahimu Juma kwa kutowafumbia macho wahalifu wa aina
yeyote ile.
Raisi Magufuli Sasa nimejua wapi kuna weakness
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment