Mbunge wa Kibamba
kupitia Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika
amewatahadharisha wananchi wa jimbo la Kinondoni kwa kutomchagua mgombea wa
CCM, Maulid Mtulia kwa madai ni msaliti na hawezi kuacha hiyo tabia.
Mnyika ametoa kauli hiyo ikiwa yupo
katika muendelezo wa kumpigia kampeni mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Salum
Mwalimu kupitia tiketi ya CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA.
"Mtulia alianza usaliti tangu
siku ya kwanza alipotangazwa kuwa Mbunge mwaka 2015, maana siku ile matokeo
yalipokuwa yanatangazwa na tume, aliposikia jina lake tu kuwa ameshinda
alikimbia na kuwaacha watu waliokuwa wakipigania atangazwe na hakutaka kusikia
matokeo ya Urais", alisema
Mnyika.
Pamoja na hayo, Mnyika aliendelea
kwa kusema "msaliti huwa haachi usaliti, hivyo kama wananchi
wakikosea na kumpa Mtulia ridhaa ya kuwa Mbunge basi atakuja kuwasaliti
tena".
Kwa upande mwingine, mpaka sasa
zimebakia takribani siku 16 ili wananchi wa jimbo la Kinondoni na Siha
kuweza kushiriki kupiga kura katika majimbo hayo ambayo yapo wazi kwa sasa.
Mnyika "Mtulia atakuja kuwasaliti Tena"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment