Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefunguka
na kudai malalamiko yaliyotolewa jana (Jumanne) na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,
Freeman Mbowe sio ya kweli bali yamejaa upotoshaji wa hali juu ambao haupaswi
kufanywa na kiongozi kama yeye.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa
tume hiyo, Kailima Ramadhani baada ya kupita siku moja tokea Mhe. Mbowe
kuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuwa Tume ya Uchaguzi iliwafanyia
hujuma katika kutoka viapo vya Mawakala wao kwenye chaguzi ndogo za marudio
Jimbo la Kinondoni na mambo mengine.
"Tume ya Taifa ya Uchaguzi
haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa bali inajibu hoja kwa
mujibu wa matakwa ya Katiba, Sheria, Kanunu na maadili ya uchaguzi na maelekezo
yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha
CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa kwa matakwa ya sheria na katiba sio
matakwa ya Mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha
siasa", amesema Kailima.
Aidha, Mkurugenzi Kailima amesema
Kanuni, Sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utaratibu wa
kushughulikia malalamiko na changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, kampeni
ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.
"Kwa masikitiko CHADEMA
walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele
walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea ndipo
walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa kwa Tume ya Uchaguzi na tume ilipitia
na ikawarudishia wagombea wao kwenda kugombea", amesisitiza Kailima.
Mkurugenzi Kailima ameendelea
kufafanua
"CHADEMA walitaka wakati wa
kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa
kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa
uchaguzi na wajumbe ni kutokea vyama vyote vilivyosimamisha wagombea na ndio
wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa tume badala ya kuwasilisha
kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote".
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa
Uchaguzi Kailima Ramadhani amemsihi Mbowe na chama chake wasome sheria za
uchaguzi na kuzielewa na kumsisitizia kuwa tume ipo tayari kumpa elimu ya mpiga
kura na kuzifahamu sheria hizo zake kwa mapana.
\
NEC yamjibu Mbowe, yamtaka akasome Vizuri Sheria
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment