Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka
Tanzania Bara Yanga SC, leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ushindi huo umekuwa ni wa kwanza kwa
Yanga ndani ya uwanja huo tangu timu ya Ndanda ipande kucheza ligi kuu soka
Tanzania bara misimu mitatu iliyopita.
Mabao ya Yanga leo yemefungwa na
kiungo Pius Buswita dakika ya 15 kipindi cha kwanza kabla ya Hassan Kessy
kuongeza bao la pil;i dakika ya 29. Baadae Yanga ilipata penalti lakini kiungo
Mkongo Papy Tshishimbi akampasia mlinda mlango wa Ndanda.
Bao la Ndanda FC limefungwa na
Nassoro Kapama dakika ya 46 kipindi cha pili lakini halikusaidia timu hiyo
kupata alama baada ya kushindwa kuongeza bao jingine hadi mpira unamalizika.
Yanga imetimiza mechi 19 za ligi
msimu huu ikijikusanyia alama 40 na kuzidi kuzikimbia Azam FC yenye alama 35 na
Singida United yenye alama 34 katika nafasi ya nne huku Simba wakiwa na alama
45 kileleni.
Yanga yaendelea kuongeza alama
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment