AZAM WACHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI


Klabu ya soka ya Azam FC kupitia kwa kocha wake msaidizi Idd Cheche imesema itaingia kwa tahadhari kwenye mchezo wao wa raudni ya 20 ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Singida United. 

“Tahadhari lazima tuingie nayo iwe nafasi yoyote uliyokuwepo lakini lazima tuingie na tahadhari kwa sababu hatutaki kufungwa tunataka kushinda kwanza'', amesema.

Cheche amesisitiza kuwa wataweka usalama katika ulinzi ili kuhakikisha mpira hauingii kwenye nyavu zao halafu watengeneze mipango ya kuhakikisha wanapata magoli ambayo yatawapa ushindi ili wazidi kuwakimbia Singida United.

Azam FC ipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35, huku Singida United ikiwa nafasi ya nne na alama 34 na zitakutana Jumamosi hii kwenye uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilipokutana zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro. Singida United ilikuwa inatumia uwanja huo kabla ya kurudi Namfua mjini Singida.


AZAM WACHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI  AZAM WACHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI Reviewed by KUSAGANEWS on February 28, 2018 Rating: 5

No comments: