Mahakama ya kijeshi nchini
Kongo imemfunga kifungo cha maisha jela ofisa wa polisi aliyemuua kwa
kumpiga risasi mshiriki wa maandamano ya kumpinga Rais Joseph Kabila.
Ofisa usajili katika mahakama ya
kijeshi Kaskazini Magharibi mwa DRC aliliambia shirika la AFP Ofisa wa polisi
Agbe Obeid amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumpiga risasi kwa
karibu na kumuua Eric Boloko Jumapili, Februari 25, eneo la Mbandaka.
Maandamano hayo yalipangwa kutokana
kwanza na kushindwa kwa Kabila kung’atuka baada ya muhula wake wa pili wa miaka
mitano kumalizika Desemba 2016 na pili kuchelewa kwa uchaguzi ambao sasa
umepangwa kufanyika mwisho wa 2018.
Boloko alikuwa mmoja wa watu wawili
walioripotiwa kuuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya mwishoni mwa
wiki katika miji ya DRC yaliyozuiwa na utawala wa Kabila lakini yaliungwa mkono
na Kanisa la Katoliki lenye ushawishi mkubwa.
Maandamano yaliyofanyika Mbandaka
Desemba 31 na Januari 21 yaliyoandaliwa na wasomi wa kanisani yalisababisha
watu 15 kuuawa baada ya kumiminiwa risasi na vikosi vya usalama.
ASKARI AFUNGWA JELA KWA KUUWA MTU KWENYE MAANDAMANO SIKU YA JUMAPILI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment