Ni mara ngapi umetuma CV kwa mwajiri
na hata kujibiwa hujajibiwa?
Tatizo inaweza ikawa sio kwamba huna
ujuzi wa kutosha, bali kwamba kuna ushindani mkubwa sana Tanzania.
Zaidi ya asilimia 10 ya watu nchini
wamekosa ajira na makampuni hupokea wastani wa maombi 100 ya kazi kwa tangazo
moja la kazi. Hivyo, CV yako lazima ijitokeze vizuri. Utaratibu wa kuomba kazi
inaweza ikawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji
uwatumie CV.
Sasa, unaweza ukafanyaje kufanya CV
yako ijitokeze zaidi ya zingine?
Kwa kuwa sisi ni rasilimali kubwa
zaidi nchini kwa waajiri kutafuta wanaotafuta kazi, kadri miaka zinavyokwenda
tumeweza kujua siri za kuandika CV safi na tutawaambia siri hizo sasa hivi.
Haswa, CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa
kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye
maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.
Sasa, vidokezo vifuatayo vitasaidia
kufanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview.
Kuwa na mpango
“Kushindwa kuwa na mpango ni mpango
wa kushindwa” – Benjamin Franklin
Unakumbuka shuleni tulifundishwa
kupanga insha zetu kabla ya kuziandika? Basi, kuandika CV ni vilevile. Kabla ya
kuiandika inabidi ufanye vifuatayo:
1.
Soma na
kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta
mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi
au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi
yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.
Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu
kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako
ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.
2.
Andika maneno
muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uzitumie kwenye CV
Usichuke sentensi nzima kutoka
kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha
na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.
Kwa mfano: Mitandao ya kijamii,
ujuzi bora wa utafiti.
3.
Fanya utafiti
juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi,
ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo
kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika
nayo. Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii
itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi
yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.
4.
Orodhesha
ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya
maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia
kufanya kazi unayoomba.
Andika
Staili inayotumika zaidi kwenye
kuandika CV ni ifuatayo:
1.
Lengo la CV na ujuzi wako
2.
Ujuzi wako wa kazi
3.
Mafanikio maalum
4.
Elimu
5.
Ujuzi muhimu binafsi
Business
Insider wanasema kwamba kwa wastani, mwajiri anaangalia CV kwa
sekunde 6 tu kabla ya kuamua kama mtafuta ajira anafaa au hafai. Kwa hiyo,
hakikisha kwamba:
1 – Zingatia staili
· Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
· Tumia size 9 – 12 ya herufi
· Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
2 – Hakikisha ni rahisi kusoma na
kuelewa
· CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
· Usitumie sentensi ndefu
Fikiria msomaji
Hakikisha CV yako inasomeka
kiurahisi na inawasilisha mafanikio yako kwa uwazi.
Tumia maneno yanayonyesha matendo
Maneno yanayo onyesha matendo
yanaonyesha kwamba wewe ni mtu wa matendo, mchapa kazi. Maneno ya aina hii ni
kama:
· Kusimamia
· Kupata
· Kuchambua
· Kusuluhisha
· Kuboresha
· Kufanya
Lengo la kutumia maneno kama haya
nikuonyesha uwezo na faida yako ndani ya mazingira ya kufanya kazi. Mwajiri
anabidi auone mchango wako wa kikazi.
Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya
hivi karibuni alafu rudi nyuma. Hakikisha una:
Ukiwa unaandika jina la kampuni
uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. Pili, eleza kwa ufupi
kampuni yao inahusika na nini. Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na
mwaka). Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu lako kwenye hilo kampuni.
Tumia nambari asilimia popote panapo
faa
Kwa mfano, badala ya kuandika
‘nilichangia ongezeko la mauzo ya kampuni’ andika, ‘nilichangia ongezeko la
mauzo ya kampuni kwa 25%’
Usidanganye
Hii ni tatizo kubwa sana Tanzania na
ukidanganya, utagundulika tu na mwajiri akifanya utafiti wake juu yako. Ni
sababu kubwa sana ya mtu kukosa ajira.
Maandalizi ya Mwisho
1.
Pitia kila
kitu kwa mara ya mwisho
Makosa ya sarufi au ya kuandika
maneno kadhaa yanaweza kusababishe ukose ajira kwa kuwa yanonyesha kwamba hauko
makini na kazi yako.
Dokezo la ziada: Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosea
yako.
2.
Rafiki apitie
CV
Muombe rafiki yako apitie CV yako.
Macho manne ni bora zaidi ya mawili!
Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi
unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba vidokezo vilivyo elezwa humu
zitakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.
Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya
kuandika CV safi, anza kutafuta kazi unayoitaka!
JUA JINSI YA KUANDIKA CV YAKO KWA UBORA ZAIDI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment