Hatimaye Bosi wa
Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani
redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi
TV’.
Diamond amevuka maji
na kuzipata leseni zake visiwani Zanzibar ambapo alikabidhiwa na Wizara ya
Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.
Mkali huyo wa ‘Sikomi’
jana aliwashirikisha mashabiki wake habari hiyo njema iliyokuwa inasubiriwa kwa
hamu, siku chache baada ya kuonesha picha akiwa anajaribu mitambo ya mradi huo
mpya.
Kupitia Instagram,
ameandika ujumbe akiambatanisha na picha za leseni hizo, akiishukuru Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
==>Diamond
ameandika:
(Leo tulikabidhiwa
Rasmi Leseni ya @wasafitv na @wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni ,
Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma…..Shukran Nyingi ziifikie
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri nzima ya Muungano wa Tanzania… Ma
raisi wetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na
Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison
Mwakiyembe….
Tamanio letu ni
kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji
ambao pengine hawajapata nafasi bado….kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi
tusingekuwepo….lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza
kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni…. )
#HiiNiYetuSote.
Ni dhahiri kuwa Wasafi
TV na Redio zitagusa anga la Tanzania Bara na Visiwani.
Diamond Akabidhiwa Rasmi Leseni ya Wasafi TV na Wasafi Redio
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment