Tanzania ni nchi yenye
walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana.
Hata kama bei
zinapanda, ulaji unaendelea kukua.
Matokeo yake ni kwamba
kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa
yanahitajika kwa wingi.
Kwa nini ufugaji wa
kuku inafaida sana?
· Kuku haina madhara mengi ya kiafya kama nyama
ya ng’ombe na watu wengi wanazidi kutambua hilo
· Kuku wanakua kwa kasi kwa hiyo unaweza ukapata
mapato makubwa kwa kipindi kifupi.
· Kuku hailiwi nyumbani tu lakini pia kwenye
migahawa, baa, hoteli na huduma zingine mbalimbali za chakula.
Kwa hiyo kama una nia
ya kuanzisha biashara ya kufuga kuku, inabidi uchukue hatua zifuatayo:
1. Chagua aina ya
kuku:
Kuna aina nyingi ya
kuku, zikiwemo:
· Kuku wa kienyeji
· Bata
· Bata Mzinga
· Kanga
· Bata Bukini
· Tombo
Kwa sasa, tutaweka
maelezo yetu kwa Kuku wa Kienyeji.
2. Amua unataka kufuga
kuku kwa malengo gani ya kibiashara
Unaweza kufuka kuku
kwa ajili ya biashara nyingi, zikiwemo:
· Kuku wa kuuza
· Kuku wa mayai
· Kuzalisha nyama ya kuku ya kuuza
· Kuzalisha chakula ya kuku ya kuuza
· Kuzalisha nyama na mayai ya kuku ya kisasa
Fanya maamuzi kwa
kuangalia kiasi cha pesa ulionayo kuanzisha biashara pamoja mahitaji ya eneo
yako.
Ni muhimu sana kufanya
utafiti wako (uliza wafugaji wengine wa kuku) kujua ni aina gani ya ufugaji wa
kuku utakaokuletea faida zaidi pamoja na gharama za kuanzia.
Kwa hapa, sisi
tunalenga ufugaji kwa ajili ya kuzalisha mayai na nyama.
3. Una pesa ya
kutosha?
Ukubwa wa shamba lako
la kuku litategemea mtaji wako. Kwa ujumla:
· Shamba ndogo itahitaji mtaji wa TZS 1.5m – TZS
3m
· Shamba ya saizi ya kati itahitaji mtaji wa TZS
4m – TZS 10m
· Shamba kubwa itahitaji mtaji wa TZS 20m au
zaidi.
4. Shamba yako itakuwa
maeneo gani?
Ukiwa unachagua eneo
ya kuweka shamba lako, zingatia yafuatayo:
· Bei ya kiwanja utakiweza?
· Gharama za kusafirisisha mayai na nyama ni za
chini? Iko karibu na soko lako na wanunuaji?
· Watu wengi wanaishi kwenye hiyo eneo? Hii
inaweza ikawa tatizo ukizingatia harufu litakalo kuwa linatoka shambani
· Kuna usalama?
Badala ya kutafuta
kiwanja kipya, watu wengi wanafunga kuku kwenye eneo lao la nyumbani. Hii inapunguza
gharama ila kabla ya kufanya hivi, kumbuka kufikiria majirani pamoja na kama
kuna kanununi za kufuata.
5. Utatumia mfumo gani
kwenye kibanda cha kuku?
Jinsi utakavyo wapanga
kuku wako kwenye kibanda chao kitachangia faida yako kwa sana.
Kuwaachia huru: Mfumo huu umetumika tangu biashara ya kufuga
kuku ulianza. Inawaachia kuku watembee wanavyopenda, ila kwa kuwaachia hivi
inaweza ikawa na madhara yake, kama:
· Mahasimu wanaweza wakawaumiza
· Watu wanaweza wakawaiba
· Kuku wanaweza wakapotea
· Magonjwa yanaweza kusambaa
· Ni ngumu zaidi kufuatilia ukuwaji wao
Ila, ni rahisi kuweka
mfumo huu na haina gharama kubwa.
Mfumo wa Chicken
Liter/Deep Litter: Hii
ni mfumo maarufu kwa shamba ndogo na za ukubwa wa kati. Kuku wanwekwa kwenye
eneo iliyozungukiwa na fensi au ukuta, alafu vipisi vidogo vidogo vya mbao
vinasambazwa chini kutumiwa kama kitanda.
Mfumo huu unamsaidia
mkulima huyu kusimamia idadi kubwa ya kuku. Ila, ubaya ni kwamba ni rahisi kwa
magonjwa kuenea.
Mfumo wa Battery
Cage: Kwa kawaida, mfumo huu
unatumika kwenye mashamba makubwa ya ufugaji kuku ila ina gharama kubwa. Kuku
wanaingizwa ndani ya ngome ya chuma, zikiwa na sehemu maalum za kula na kunywa
maji. Pia, kuna nafasi maalum ya kutaga. Kwa kuwa idadi ya kuku wanaowekwa
kwenye kila ngome sio kubwa, ni rahisi kujua kuku yupi anaumwa au hatagi.
6. Unahitaji vifaa
gani?
Zaidi ya kuwajengea
kibanda, kuku wako watahitaji vifaa vingine kama:
· Vifaa vya kunywa
· Vifaa vya kula
· Viota
· Taa
· Makreti
· Inkubeta
· Pechi
· Mfumo wakutoa takataka
· Trei ya mayai
· Hita
· Ngome
7. Utawalisha nini
kuku wako?
Je, utanunua chackula
chao au utiakitengeneza mwenyewe?
Kutengeza chakula cha
kuku kinahitaji mtaji mkubwa zaidi, ila, kadri muda unavyoenda, gharama yake
inakuja kuwa china ya kununua chakula chao kila mara ikihitajika. Pia, unaweza
ukajiongezea mapato kwa kuwauzia wafugaji wengine wa kuku.
Mwisho wa siku maamuzi
yatategemea na kufanya utafiti wa zote mbili na kujua gharama zake dhidi ya
maslahi yako.
8. Inabidi umwajiri
mtu?
Kama ufugaji wa kuku
haitakuwa kazi yako ya kudumu, utahitaji kumwajiri mtu/watu kukusaidia na
usiamamizi. Baadhi ya watu utakawahitaji ni:
· Msimamizi wa biashara kwa ujumla
· Mhasibu
· Msimamizi wa kuku
· Mlinzi
· Mtu wa kutangaza biashara yako – we unaweza
kufanya kazi hii. Itabidi utafute namna ya kutangaza biashara yako kwenye
intaneti kwa kupitia orodha za
biashara kama iliyopo ZoomTanzania, kwenye mitandao ya kijamii, kwa
kuchapisha vipeperushi n.k
9. Chanjo za kuku na
upimaji wa afya mara kwa mara
Kadri biashari yako
itakavyokuwa, ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa mganga wa mifugo na kuchanja
kuku wako kuzuia magonjwa kusambaa.
Kumbuka, afya ni
muhimu kuliko bei ya kuku wako. Ila, weka bei inayoeleweka.
Biashara inayolipa
Kufuga kuku inahitaji
subira na kujitolea ila, faida zikianza kuingia utafurahi sana!
Jua Jinsi ya Kuanzisha Biashara Ya Kufuga Kuku Yenye Mafanikio
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment