Mbunge wa
Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe ameishauri Serikali iweke mazingira
rafiki na bora kwa sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya uchumi wa Taifa.
Ametoa ushauri
huo jijini Mwanza leo Jumatano Januari 24,2018 wakati wa kipindi cha
Tujadiliane kinachoandaliwa na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini
(UTPC).
Zitto ambaye
pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo amesema, “Tuongeze uzalishaji na kuuza nje
kuliko tunavyoagiza na tuwekeze kwenye miradi yenye kugusa maisha na uchumi wa
mwananchi moja kwa moja.”
Amesema ujenzi
na uboreshaji miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga ni muhimu,
lakini uendane na shughuli zinazozimua na kusisimua uchumi kwa kuongeza
uzalishaji wa bidhaa za sekta ya kilimo ili kuvihakikishia malighafi viwanda
vya ndani.
Kabla ya
kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli, tungewekeza kwenye uzalishaji wa chuma kule
Liganga na Mchuchuma. Hii si tu ingetumika kama malighafi kwenye mradi wa
ujenzi wa reli nchini, bali pia katika nchi jirani za Kenya na Rwanda ambazo
pia zinawekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya reli,” amesema.
Akizungumzia
utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025, Zitto amesema
suala hilo linapaswa kufungamanishwa na uzalishaji wa mazao ya kilimo kama vile
pamba, korosho, michikichi na mengine yatakayotumika kama malighafi.
Ameshauri
uwekezaji wa fedha, teknolojia na maarifa katika sekta ya kilimo inayoajiri
zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania kwa kutoa ruzuku kwa wakulima ili pamoja na
kuongeza uzalishaji, pia iwahakikishie fidia bei inaposhuka katika soko la
dunia na mafao ya uzeeni wanapokosa uwezo wa kuendelea kulima.
“Wafanyakazi
wanalipwa mafao wanapostaafu. Je, mkulima anapozeeka na kukosa uwezo wa kulima
anapata wapi mafao?” amehoji Zitto.
Akijibu swali
kuhusu maisha yake baada ya siasa, amesema anakusudia kuwa mhadhiri katika
taasisi za elimu ya juu na kuandika vitabu vya kiuchumi, kitaaluma na harakati
za kisiasa.
ZITTO KABWE AISHAURI SERIKALI KUHUSU UCHUMI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment