Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameivunja Serikali
ya Kijiji cha Emboreet wilayani Simanjiro, kwa kukwamisha shughuli za maendeleo
kwa sababu ya madai ya Sh30 milioni ya posho ya vikao.
Mnyeti amefikia uamuzi huo baada ya wajumbe 14 wa serikali
ya kijiji hicho kudai Sh30 milioni za posho ya vikao jambo alilosema halipo
kisheria.
Amesema wajumbe hao waliamua kila mmoja alipwe Sh30,000 za
posho ya kikao, huku mwenyekiti wa kijiji hicho, John Olendikoni akilipwa
Sh40,000.
Mnyeti amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Simanjiro, Yefred Myenzi hakuidhinisha malipo hayo hivyo kuwa chanzo cha
kukwamisha maendeleo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia alituhumiwa
kufuja Sh4 milioni alizirudisha na baadaye alijiuzulu nafasi hiyo mbele ya mkuu
wa mkoa.
Mnyeti amemwagiza Myenzi kuitisha uchaguzi mpya kujaza
nafasi hizo baada ya siku 30 kuanzia jana Jumanne Januari 23,2018.
RC MNYETI AVUNJA SERIKALI YA KIJIJI CHA EMBOREET SIMANJIRO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment