Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza kuwekwa mahabusu mratibu wa
mradi wa ufugaji samaki wilayani Ukerewe, Jackson Ndobeji kwa mahojiano kuhusu
ubadhirifu na utekelezaji mradi chini ya kiwango.
Lugola ametoa agizo hilo baada ya kukagua mradi huo unaotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la
Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa gharama ya Sh317.4 milioni.
UNDP inafadhili miradi ya ufugaji samaki katika Kijiji cha
Namagondo wilayani Ukerewe tangu mwaka 2014.
“Pamoja na mratibu kukamatwa, naagiza uchunguzi na hatua za
kisheria dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu katika mradi huu,”
amesema Lugola.
Amesema ziara kwenye miradi mingine ya aina hiyo katika
wilaya za Bahi na Kongwa mkoani Dodoma imebaini imetekelezwa chini ya kiwango
licha ya kugharimu mamilioni ya fedha.
Awali, katibu wa kikundi cha Pambazuka chenye wanachama 13,
Athanas Musiba alimweleza Lugola kuwa baadhi ya waliostahili kupokea fedha
hawajapatiwa chochote kutoka timu ya uratibu.
Akizungumza kabla ya kushikiliwa na polisi, Ndobeji alidai
ofisi yake imepokea Sh240 milioni zilizotumika kujenga mabwawa, nyumba ya
mlinzi na matangi ya maji kwenye eneo la mradi.
Bila kutaja kiasi, alisema fedha zingine zimetumika kununua
vifaa vya umeme jua kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya mradi.
Ndobeji amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasili Ukerewe
wakati wowote na kwamba, wameomba fedha ili kukamilisha kazi iliyosalia
NAIBU WAZIRI AAGIZA MRATIBU WA MRADI KUWEKWA MAHABUSU KWA UZEMBE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment