Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC),
umeiomba Serikali kuhakikisha mwandishi wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi
Communications Limited (MCL), Azory Gwanda anapatikana.
Azory alichukuliwa na watu wanne waliokuwa kwenye gari jeupe
aina ya Toyota Land Cruiser, Novemba 21,2017 katika mji wa Kibiti mkoani
Pwani alikokuwa anaishi na kufanya kazi.
Mkurugenzi wa umoja huo, Abubakar Karsin ametoa kauli hiyo
leo Jumatano Januari 24,2018 wakati wa mahojiano na mbunge wa Kigoma Mjini
(ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe katika kipindi cha tujadiliane kinachoandaliwa na
umoja huo na kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari.
“Mwanzoni walianza kupotea watu wa kada zingine sasa imefika
kwa waandishi wa habari. Hatujui zamu ya nani inafuata,” amesema Karsan
Amesema hofu ya kuminywa kwa uhuru wa habari na maoni
ulioikumba sekta ya habari nchini usipodhibitiwa utaunyima umma fursa ya kupata
habari, hivyo kupunguza uwezo wa wananchi kushiriki, kujadili na kuamua masuala
yanayowahusu.
Amebainisha kuwa, sekta ya habari nchini bado ina kumbukumbu
ya kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel
ten, Daud Mwangosi aliyeuawa mikononi mwa polisi
Karsan amesema kupotea kwa Azory kunatia chumvi maumivu ya
wanahabari
Kuhusu ukusanyaji wa habari, Karsan amemwomba Zitto
kuwasilisha ombi la wanahabari kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba ili awaeleze makamanda wa polisi wa mikoa kuondoa urasimu wa utoaji
habari zinazohusu matukio ya jinai na uhalifu.
VILABU VYA WANDISHI WA HABARI WAOMBA MWANDISHI WAWANANCHI ARUDISHWE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment