Wanafunzi 229
wa Shule ya Msingi Mitambo wilayani Mtwara wanasoma wakiwa chini ya miti
kutokana na uhaba wa madarasa matano
Akizungumza mwalimu
mkuu wa shule hiyo, Rashidi Chalilo amesema wanafunzi hao ni kati ya 436 wa
shule hiyo.
Chalilo
amesema wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kutokana na kuhitaji uangalizi
zaidi wanasoma darasani pamoja na wa darasa la saba wanaojiandaa kwa mitihani.
Amesema shule
hiyo ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na wanafunzi 99 na sasa wapo 436 ikiwa na
madarasa matatu pekee.
Mwalimu mkuu
huyo amesema wazazi walijenga madarasa ya muda kwa kutumia miti na udongo na
kuyaezeka kwa nyasi lakini baadaye yalibomolewa kwa maelekezo ya
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili kupisha ujenzi wa madarasa ya kudumu
Akizungumzia
suala hilo, kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji cha Mitambo, Ally Mselemu amesema
wanasubiri kupelekewa saruji na vifaa vingine vya ujenzi.
Wananchi tuko
tayari kujitolea nguvu kazi kuboresha shule yetu, hivyo tunaiomba Serikali
ituletee vifaa,” amesema Mselemu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Omari Kipanga amesema wameshatenga
fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu pamoja na nyumba ya mwalimu.
Amesema Sh156
milioni zimetengwa kutoka katika mfuko wa elimu ambazo zinatokana na mapato ya
korosho
Kipanga
amesema mfuko wa P4R pia umeidhinisha Sh326 milioni kwa ajili ya kuboresha
sekta ya elimu katika halmashauri hiyo
Uhaba wa madarasa wasababisha 229 kusoma chini ya miti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment