Mwalimu mmoja wa sekondari nchini Kenya
Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa mahakamani kwa
kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja kwa panga.
Wakielezea mbele ya mahakama
mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya
usalama Kaunti ya Kirinyaga, Maina Muriuki walimweleza Jaji Lucy
Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa huyo alivyoua mtoto wake,
Bwana Maina aliieleza mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa
umeeekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Bw Wangara, na kando ya
mwili huo kuliwa na panga ambayo ilitumiwa kumuua mtoto huyo.
Shahidi mwingine Joseph Muriithi alisema wakati wa tukio hilo alikuwa
shambani kwa Bw. Wangara akifanya kibarua, na mtuhumiwa huyo kwenda akiwa na
madoa ya damu, na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya
mwalimu huyo.
Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Machi 1, 2018, ambapo
itasikilizwa tena.
Bw Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba wa watoto wawili na
mwalimu katika shule ya upili (sekondari) ya Gituya
AUWA MTOTO WA MIEZI SABA KWA KUMCHINJA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment