Nchini Kenya mamia ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya
Jamhuri jijini Nairobi wameingia katika mvurugano mkubwa kufikia hatua ya
kuchomana visu baada ya usiku wa jana kutokea vurugu ya kidini kwenye shule
yao.
Ambapo vyombo vya habari nchini humo vimeripoti taarifa hiyo na
kueleza kuwa ugomvi huo umetokea kati ya wanafunzi wa kiislamu na wakikristu
ambao walikuwa wakibishana kuhusu dini zao..
Kwenye mzozo huo Wanafunzi wa dini ya Kiislamu walikuwa
wanawalazimisha wenzao wakristo kubadilisha dini (Kuslimu) na ndipo vurugu
zilipoanzia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa vurugu hizo zimetokea usiku wa
kuamkia leo na mamia ya Wanafunzi wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu huku vitanda
na madawati yakivunjwa kwenye vurugu hizo.
Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi jijini Nairobi limefika
shuleni hapo asubuhi hii kufuatilia tukio hilo ili kutoa taarifa rasmi idadi ya
wanafunzi waliojeruhiwa.
Wanafunzi wachomana visu kwa kubishania dini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment