Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akishtakiwa kwa kesi mbili.
Katika kesi moja anadaiwa kuchoma moto nyumba ya Mary Tesha
aliyokuwa akiishi Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Alphonce Muyinga
Mchungaji Msigwa ambaye ni mshtakiwa wa saba katika kesi
zote mbili amefikishwa mahakamani leo Jumatano Januari 24,2018 baada ya
kuripoti kituo kikuu cha Polisi.
Katika kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018 mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi, David Ngunyale, Wakili wa Serikali, Felix Chakla
amedai kati ya Januari 5 na 14,2018 washtakiwa walipanga njama za
kuharibu mali.
Pia wanadaiwa Januari 15,2018 walibomoa nyumba
ya Anjelus Mbogo aliyekuwa diwani wa Mwangata aliyejiuzulu kutoka Chadema
na kuhamia CCM.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwenyekiti wa Baraza
la Vijana la Chadema Iringa Mjini, Leonce Marto; diwani mteule wa Viti Maalumu,
Rehema Mbeta na Patrick Madati
Mchungaji Msigwa na wenzake wako nje kwa dhamana baada ya
kila mmoja kusaini bondi ya Sh2 milioni.
Katika kesi ya pili, Mchungaji Msigwa na wenzake sita
wanadaiwa kupanga njama ya kutenda uhalifu kinyume cha sheria.
Wakili Chakla mbele ya hakimu Ngunyala amedai Januari
17,2018 washtakiwa kwa pamoja walichoma nyumba ya Tesha aliyokuwa akiishi
Muyinga.
Kwa shauri hilo namba 7 la mwaka 2018, washtakiwa wanadaiwa
Januari 17,2018 waliichoma moto nyumba hiyo iliyopo kata ya Kihesa katika
Manispaa ya Iringa.
Washtakiwa walikana kosa na hakimu Ngunyale aliwaachia
kwa dhamana baada ya kila mmoja kudhaminiwa na wadhamini wawili waliosaini
bondi ya Sh3 milioni.
Mchungaji Msigwa na wenzake katika kesi hizo wanawakilishwa
na wakili wa kujitegemea Anthony Rutebuka. Hakimu Ngunyale ameahirisha kesi
hizo hadi Februari 2,2018
Peter Msigwa na wenzake 12 wafikishwa mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment