Kamanda wa polisi mkoa
wa kipolisi Kinondoni RPC, Muliro Jumanne Muliro awaonya na kuwataka wasiasa
kufanya kampeni zao kistaarabu bila kuvunja sheria za nchi zinavyoelekeza na
kuacha kutumia lugha zisizo na staha katika kampeni zao.
Akizungumza leo Jijini Dar es
salaam kamanda Muliro amesema wamejipanga kuhakikisha chaguzi wa Jimbo la
Kinondoni hauna nafasi yakuvunja amani na sheria za nchi kwakua taratibu na
kanuni zilizowekwa na serikali zinafuatwa na hawatasita kumchukulia hatua za
kisheria mtu yeyote atakayeonekana kukiuka sheria za nchi.
Kamanda Muliro amesema wanatambua umuhimu wa zoezi hilo hivyo
watagawa askari kulingana na ukubwa wa eneo na wingi wa wapiga kura.
WANASIASA WAONYWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment