Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye
thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila
zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na
dududu 11.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"
Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua
Aidha Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa mapato.
Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.

ZANA HARAMU ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 30 ZATEKETEZWA GEITA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment