WALIMU 2 WASHUSHWA VYEO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LA RAISI



MKUU wa wilaya ya Kibaha,Mkoani Pwani, Assumpter Mshama ameamuru walimu wawili wa shule za msingi washushwe vyeo kutoka nafasi ya mwalimu mkuu na kuwa walimu wa kawaida ,kutokana na kosa la kuchangisha michango wazazi.

Hatua hiyo ,ameichukua siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,kukemea tabia inayofanywa na baadhi ya walimu wakuu na bodi za shule kuchangisha wazazi na walezi michango ambayo serikali imeizuia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha ,alisema walimu hao wamekiuka agizo la serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk .John Magufuli.

Mshama aliwataja walimu hao kuwa ni mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembesaba, Rashinde Kilakala ambaye alikuwa akipokea sh.1,000 kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya mitihani jambo ambalo ni kinyume cha agizo la serikali.

Mwalimu mwingine ni wa shule ya msingi Jitegemee, Sapiensia Kilongozi ambae aliweka kikao na kuita wazazi na kuwataka wazazi wenye watoto watoe shilingi 2,000 kwa wiki kwa ajili ya masomo ya ziada na mitihani.

Mshama alisema,huo ni mwanzo kwani ataendelea kusimamia maagizo yanayotolewa na serikali ili iwe fundisho kwa walimu wanaokaidi mipango ya serikali hiyo.

Alieleza atakaeendelea kufanya hivyo akibainika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi
WALIMU 2 WASHUSHWA VYEO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LA RAISI WALIMU 2 WASHUSHWA VYEO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LA RAISI Reviewed by KUSAGANEWS on January 21, 2018 Rating: 5

No comments: