Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania kujitokeza
kumchangia msanii wa Filamu Wastara Issa ili aweze kwenda kupatiwa matibabu
India ya mguu wake unaomsumbua.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito
huo alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu nyumbani kwake leo Tabata
Sanene jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu
wake uliyokatwa mpaka kufikia kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.
|
|
Ndugu zangu watanzania najua kutoa
ni moyo na siyo utajiri ninawaomba mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani
mpaka sasa anahitaji kiasi cha milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha
safari yake hiyo ya kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye
matibabu hayo mwezi ujao
|
|
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa wito kwa wasanii wote wa filamu nchi
kujitokeza na kumsadia mwanatansia mwenzao wa filamu katika kufanikisha
anapata matibabu ili aweze kurudi na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida
|
|
Bodi ya Filamu nchini kwa
kushirikiana na Baraza la Sanaa laTaifa tumetoa kiasi cha shilingi Milioni
moja kwa ajili ya kumchangia katika kufanikisha safari yake ya matibabu na
serikali kwa ujumla inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha msanii
huyu anapata kiasi hicho cha pesa kilichobakia
|
|
Pamoja na hayo Katibu Mtendaji
BASATA Bw.Godfrey Mngereza alitoa wito kwa wasanii wote nchini kwa nao
kijitokeza kumchangia msanii huyo kwani wasanii wote ni wamoja kwa maana wote
ni wanafanya kazi ya sanaa hivyo ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.
|
|
Kwa upande wa msanii Wastara Issa
aliishukuru serikali kwa kumtembelea na kumjulia hali pamoja na kumchangia na
kusema imekuwa nifaraja kubwa kwake kuwaona na alitoa akaunti namba
anayotumia kwa ajili ya kukusanyanyia michango ambayo ni EQUITY BENKI 82113007111415583 na namba za simu anazotumia kuchangisha ni 0768 8211; 666 113 na 0713 666 113 na alieleza amesajiliwa kwa jina la
Wastara Issa katika namba hizo za simu pamoja na akaunti namba yake.
|
|
|
DOKTA MWAKYEMBE AOMBA WATANZANIA KUJITOLEA KUMSAIDIA WASTARA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment