MBUNGE wa Jimbo la Kasulu
Vijijini, Agaustine Vuma ameahidi
kufanya ziara ya kutembelea vijijini vyote vya jimbo hilo kwa lengo la
kuangalia changamoto na kero zinazo wakabili wananchi
Amefafanua changamoto atakazokutanazo baada
ya kuwasikiliza wananchi wake, hatua itakayofuata ni kuzifikisha Serikali
zitatuliwe ili waendelee kufurahia uongozi wao uliopo madarakani.
Vuma amesema hayo jana wakati akikagua
miradi inayotekelezwa katika jimbo hilo ikiwemo mradi wa Kituo cha Afya cha
Nyakitonto kilichotengewa Sh. milioni 500.
Ambapo mpaka sasa ujenzi huo umekamilika kwa
asilimia 70 mpaka sasa na fedha Ilizo tumika ni Sh.milioni 290,"amefafanua
Vuma.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa
ajili ya kutatua changamoto za wananchi na ndio maana Rais,Dkt.John Magufuli
ameanza kuboresha sekta za afya kwa kutoa fedha katika vituo vya afya.
Ameongeza lengo la fedha hizo ni kuhakikisha
wananchi huduma za afya vizuri pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na afya
njema.
Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kuendelea
kuwasaidia wananchi na sisi kama wawakilishi kazi yetu ni kuibua matatizo na
kumpelekea aweze kuyatatua.
"Mpaka sasa tunaendelea kuboresha
huduma za afya na nimeahidiwa kupewa fedha nyingine kwaajili ya kituo cha afya
Rusesa na fedha hizo zitaendelea kutolewa kwa kuwa ni utekelezaji wa Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi(CCM)", amesema Vuma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kasulu Vijijini ambae pia ni Diwani wa kata ya Nyakitonto , Yohana
Mshita amesema wananchi wa vijiji vilivyo karibu na kata hiyo walikuwa
wakiteseka kupata huduma.
Amesema wananchi wengine walikuwa
wakilazimika kufuata huduma Kasulu Mjini na kusababisha kupoteza nguvu kazi
lakini kwa sasa wataendelea kupata huduma karibu.
Ameongeza fedha zilizotolewa zimetumika
kujenga chumba cha upasuaji, wodi za Wagonjwa, nyumba ya Mganga na chumba cha
kuhifadhia maiti.
Amesema mpaka sasa kuna fedha nyingi
zimebaki, na wataendelea kuzihifadhi ili zitumike katika miradi mingine itakayo
ibuliwa na wananchi
Nao baadhi ya wananchi, akiwamo Happynes
Dastan amesema wamekuwa wakililia kupata kituo cha afya karibu kwani walikuwa
wakilazimika kufuata huduma za upasuaji Wilaya ya Kasulu.
Sasa tunauhakika wa kupata huduma za afya
hapa hapa na kuendelea kufurahia huduma hiyo kwa karibu,"amesema.
Amesema wanampongeza sana Rais wa Magufuli
kwa kazi kubwa anayoifanya na shughuli ya kuwahudumia wananchi wanyonge kwa
shida walizokuwa nazo.
MBUNGE WA KASULU VIJIJINI AWASOGOLEA WANANCHI NA KUPATA KERO ZAO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment