Wilaya
ya Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo haina hospitali ya Wilaya imejipanga
huhakikisha inaanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo.
|
Wilaya ya Simanjiro iliyoanzishwa mwaka 1993 baada ya kugawanywa
kutoka wilaya ya Kiteto, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ina wananchi 178,693
lakini hadi hivi sasa haina hospitali ya wilaya.
Myenzi
alisema viongozi na wananchi wa wilaya hiyo kwa pamoja wanapaswa kushikamana
ili kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa hospitali hiyo ya wilayani.
|
Alisema
ameshakutana na wataalamu wa idara ya afya waliotoka ofisi ya Rais Tamisemi,
waliofika ofisini kwake na kupanga mipango ya kuanzisha hospitali ya wilaya
hiyo.
|
"Sikubaliani
na pendekezo la kukipandisha hadhi kituo cha afya Orkesumet ili kiwe
hospitali ya wilaya, hapana tunapaswa kujenga hospitali ya wilaya na kituo
cha afya Orkesumet kitaendelea kufanya kazi yake kama kawaida," alisema
Myenzi.
|
Alisema
tangu wilaya hiyo ya Simanjiro ianzishwe haijawahi kuwa na hospitali ya
wilaya, hivyo huu ni wakati muafaka wa kuanza mchakato wa ujenzi wake.
|
Diwani
wa Kata ya Orkesumet, Sendeu Laizer alisema anaunga mkono hatua ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yefred Myenzi kuanza ujenzi wa
hospitali mpya ya Wilaya na kutopandisha hadhi kituo cha afya cha Orkesumet.
|
Laizer
alisema suala hilo ni maendeleo makubwa kwa wananchi wa kata ya Orkesumet na
Wilaya ya Simanjiro kwa ujumla kwani wilaya hiyo haijawahi kuwa na hospitali
ya wilaya tangu ianzishwe
|
Mkazi
wa Orkesumet, Baraka John alipongeza jitihada za Myenzi kuanzisha mchakato wa
ujenzi wa hospitali hiyo kwani anaamini mikakati hiyo itafanikiwa
|
"Tunaposema
uongozi wa ubunifu na unaoacha alama ni huu alioufanya mashine ya kazi Myenzi
kwani hospitali ya wilaya ni hitaji la muda mrefu kwa jamii ya eneo
hili," alisema John.
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Yefred Myenzi
akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole na Katibu
Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary.
|
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Albert Msole akizungumza
wakati akifungua kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, kulia ni
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo Yefred Myenzi.
|
SIMANJIRO YANZA MPANGO WA KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment