Klabu ya soka ya Yanga
imetoa sababu kwanini mlinzi wake mpya wa kimataifa Fiston 'Festo' Kayembe
Kanku ameshindwa kujiunga na timu tangu asajiliwe Disemba 2017.
Akiongea leo Mwenyekiti wa
Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika amesema mchezaji huyo raia wa DR
Congo hajajiunga na timu kwasababu anashughulikia matatizo ya kifamilia.
“Kanku ana matatizo makubwa ya kifamilia ndiyo maana tumempa
ruhusa ya kwenda kuyashughulikia, akimaliza atakuja kuanza kazi, na atacheza tu
ligi bado ina mechi nyingi sana,”amesema Nyika.
Kwa upande mwingine Nyika ameongelea suala la uhamisho wa
kimataifa (ITC), amabapo ameeleza kuwa ulikuwa unasumbua ila kwasasa wapo
kwenye hatua za mwisho kuupata japo kuwa tayari mchezaji huyo ni mali ya
Yanga.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara wanashika
nafasi ya 5 kwenye msimamo wakiwa na alama 22 kwenye mechi 13 walizocheza huku
kesho wakishuka dimbani kucheza na Ruvu Shooting.
Yanga yamtetea beki wake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment