Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Isack Kamwelwe amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Kitila
Mkumbo kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Clement Kivegalo.
Pia, Kamwelwe amemwagiza
mkurugenzi wa utawala wa wizara hiyo, Barnabas Ndunguru kuwahamishia
Dodoma watumishi 178 wa wizara ifikapo Januari 30, 2018 la sivyo atamchukulia
hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Januari 20, 2018 jijini Dar es Salaam, Waziri Kamwelwe amesema jana
Januari 19, alizivunja bodi za maji safi za Mkoa wa Arusha na Musoma
baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wao si mzuri.
Juzi tu niliuondoa utendaji wa
Lindi, kuna tatizo la utendaji wa wakandarasi hapa Dar es Salaam, Chalinze na
tuna tatizo Kigoma, mamlaka za maji za miji ya mikoa zinasimamiwa na
mkurugenzi wa maji mijini, hapa tuna idara kama tatu au nne zinasimamia
utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Mhandisi Kamwelwe na kuongeza,
Idara ya maji mijini inaongozwa na
Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Clement Kivegalo wakati haya yote yanatokea
Kivegalo yupo lakini matatizo yanatokea yanabainiwa na waziri, naibu waziri
au katibu mkuu, leo Januari 20, 2018 namwagiza Katibu Mkuu atengue uteuzi
wake atafute mtu mwingine.”
Waziri Kamwelwe amesema Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa aliyeko ziara mkoa wa Mara amebaini kasoro za utendaji
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa) na kuagiza
hatua zichukuliwe ikiwamo kuchunguzwa watendaji wote.
Kupitia ziara ya Waziri Mkuu
imebainika yapo matatizo yanayomhusu mkurugenzi wa Muwasa, Gantara Said na
wahusika wote ameeleza wafanyiwe uchunguzi, hivyo kuanza leo Januari 20,
natengua uteuzi wake na nafasi yake itakaimiwa na Petro Muhoja wa Mamalaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza, namwagiza mkurugenzi wa mamalaka ya
maji Mwanza, asaidie mamlaka ya maji Musoma ili waweze kufanya kazi,”
amesema.
|
Waziri wa Maji aagiza kaimu mkurugenzi wa maji asimamishwe kazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment