WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa
mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama.
Amekagua
shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari
20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama.
Waziri Mkuu
amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora
za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.
Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho
hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima
zao hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho
Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na
mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.
Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo
zinazozalishwa katika shamba hilo zitagawanywa kwa wakulima katika kata zote 18
za wilaya ya Butihama.
Alisema mbali ya kuzalisha mbegu pia wanatarajia kuanzisha
kiwanda cha kuchakata zao la mihogo ili kuweza kuliongezea thamani.
Mbali na shamba la mbegu bora za mihogo pia kikosi hicho
kina shamba lingine la pamba lenye ukubwa wa ekari 57, ambapo wanatarajia
kuvuna tani 57 za pamba. Mwakani wanatarajia kuongeza ukubwa wa shamba na
kufikia ekari 300.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea shamba darasa la mkoa wa
Mara la zao la pamba lililopo Kisangwa wilayani Bunda akiwa njiani kuelekea
wilayani Butihama, kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima alisema shamba darasa hilo
ni moja ya jitihada za Mkoa wa Mara kuelimisha wakulima wa zao hilo mbinu bora
za uzalishaji ili kuongeza tija katika uzalishaji.
WAZIRI MKUU ATEMBELEA SHAMBA LA JKT RWAMKOMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment