WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Halmashauri
na Mji wa Bunda pamoja na Madiwani washirikiane katika utekelezaji wa ujenzi wa
miradi ya maendeleo.
Pia
amewaagiza watumishi wa umma katika halmashauri ya wilaya na mji wa Bunda
wafanye kazi kwa bidii na wawahudumie wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi
na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na wa Halmashauri Mji wa Bunda, katika
ukumbi wa Halmashauri ya Bunda.
“Watumishi wa
umma acheni kukaa sana maofisini tengeni muda wa kuwatembelea wananchi
katika maeneo yao na shirikianeni nao katika kutatua kero zinazowakabili.
Madiwani na watumishi lazima mshirikiane ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema watumishi na madiwani wakishirikiana katika usimamizi wa
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, wilaya itafanikiwa katika
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Pia Waziri Mkuu aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa
mujibu wa sheria na taratibu za utumishi na wajiepushe na vitendo vya
rushwa, wizi , ufisadi na uzembe kwa sababu vinarudisha nyuma maendeleo ya
wananchi.
Awali, Waziri Mkuu alikagua mradi wa maji wa Bunda na
baadae alizindua kikundi cha Ushirika cha Igembe Sabo na kukagua skimu ya
umwagiliaji wa zao la mpunga ya Nyatwali wilayani Bunda.
Waziri
Mkuu alihitimisha ziara yake wilayani Bunda kwa kuhutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Stendi Mpya katika mji mdogo wa Bunda.
WATUMISHI NA MADIWANI SHIRIKIANENI KATIKA MAENDELEO -MAJALIWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment