Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi
la Polisi nchini kutafuta namna ya kupunguza wahalifu wanaokamatwa kwa makosa
kama uzururaji ili kupunguza mrundikano kwenye mahabusu.
Ameeleza kuwa suala hilo pia litaepusha watuhumiwa
wanaopelekwa mahabusu kwa makosa ya uzururaji kupata nafasi ya kuzungumzia
masuala ya uhalifu na watuhumiwa waliozoea.
Kwa upande mwingine Dr. Mwigulu ameagiza wananchi
kushirikiana na serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la
ulinzi ni ajenda ya kila Mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele.
Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
Dr. Mwigulu amesema kuwa mkakati wa Halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa
cha polisi ni kitendo cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina
zote.
Ameeleza kuwa suala hilo pia litaepusha watuhumiwa wanaopelekwa mahabusu kwa makosa ya uzururaji kupata nafasi ya kuzungumzia masuala ya uhalifu na watuhumiwa waliozoea.
Kwa upande mwingine Dr. Mwigulu ameagiza wananchi kushirikiana na serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la ulinzi ni ajenda ya kila Mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele.
Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Dr. Mwigulu amesema kuwa mkakati wa Halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa cha polisi ni kitendo cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina zote.
MWIGULU POLISI TAFUTENI NAMNA NYINGINE YA KUSHUGHULIKA NA WAZURURAJI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment