Mabingwa watetezi wa
ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1
kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 15 dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Azam
Complex.
Yanga ilitokea nyuma ikisawazisha
bao la mapema la Azam FC liliofungwa dakika ya 4 na mshambuliaji Shabaan
Chilunda baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Yanga.
Mshambuliaji raia wa Zambia ambaye
alikuwa amefungiwa mechi tatu Obrey Chirwa, leo alikuwa anarejea baada ya
kumaliza adhabu yake hiyo na alifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 30
akitumia vizuri makosa ya mlinda mlango wa Azam FC Razak Abarola.
Mlinzi wa kushoto wa Yanga
aliyesajiliwa msimu huu akitokea Azam FC Gadiel Michael ndiye aliyeimaliza Azam
FC dakika ya 44 kwa kufunga bao la pili kupitia mkwaju wa mbali ambao
ulimshinda mlinda mlango wa timu yake hiyo ya zamani.
Baada ya ushindi wa leo Yanga sasa
imefikisha alama 28 na kuikaribia Azam FC yenye alama 30 katika nafasi ya pili
nyuma ya Simba SC yenye alama 32 kileleni.
YANGA YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA AZAMA FC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment