Mwanasiasa mkongwe na
aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika serikali ya awamu ya nne
na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Stephen Wasira amedai hawawezi
kufanya siasa bila ya kukitaja chama cha CHADEMA kwa kuwa ndio shetani wao
Wasira amebainisha hayo leo wakati
wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika katika
viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo
ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba baada ya kusikia kauli ya mgombea Ubunge wa Jimbo
hilo katika 'televison' kuwa CCM hawawezi kufanya siasa bila ya kuitaja
CHADEMA.
"Nimemshangaa kiukweli mgombea
huyo, maana hata Maimamu na Wachungaji huwa hawawezi kumaliza ibada bila ya
kumtaja shetani maana shetani ndio mpinzani wao na endapo wasipotaja wana kuwa
hawajamaliza ibada yao. Hivyo asishangae sana na sisi tunapokuwa katika siasa
kuitaja CHADEMA kwa maana ndio shetani wetu hapa", alisema Stephen Wasira.
Kwa upande mwingine, Wasira amesema
tokea mwaka 2015 kumekuwa na siasa za kishetani nchini Tanzania hasa upande wa
upinzani ambazo zimetawaliwa na uongo unaofanana na giza kwa kusema uongo
katika kampeni zao na kudanganya wananchi.
WASIRA"HUWEZA KUFANYA SIASA BILA KUTAJA CHADEMA MANA NDIYO SHETANI WETU"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment