Mbunge wa Ubungo, Said
Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amesema mgombea
wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu
makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.
Kubenea amesema hayo leo Januari 27,
2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa
kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha, Kubenea
amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika
Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.
"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni
kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa
wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo
makubwa sana na kutetea hazi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi
ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine,
mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea
Mbali na hilo Kubenea aliwataka
wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na
kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na
maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi.
KUBENEA MGOMBEA UBUNGE KINONDONI NDIYE LISU MDOGO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment