Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos
Makalla ameunda kamati maalum ya watu kumi kuchunguza utata wa utekelezaji wa
mradi wa ujenzi wa ofisi mpya za halmashauri ya wilaya ya Chunya wenye thamani
ya shilingi Bilioni 4.8 ambao umesimama tangu mwezi julai mwaka jana huku
kazi ambayo imefanyika ikidaiwa kuwa hailingani na thamani ya fedha iliyolipwa
kwa mkandarasi.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi mpya za
halmashauri ya wilaya ya Chunya, ambako ameshuhudia mradi huo ukiwa umesimama
tangu mwezi julai mwaka jana na ndipo akaomba kupewa maelezo kuhusu sababu za
mradi huo kusimama pamoja na kiasi cha fedha kilicholipwa.
|
Baada ya kusikiliza maelezo hayo,
mkuu huyo wa mkoa hakuridhika na mwenendo wa utekelezeji wa mradi huo hususan
kiwango cha fedha kilicholipwa kwa mkandarasi ikilinganishwa na kazi
iliyofanyika na ndipo akaagiza mkandarasi anayefanya kazi hiyo afike mara moja
kwenye eneo la kazi, huku akiamua kuunda kamati ya watu 10 kuchunguza mradi
huo.
|
|
Kamati hiyo ya watu kumi ambayo
imetangwazwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya,Amos Makalla, inahusisha wajumbe kutoka
taasisi mbalimbali za serikali mkoani Mbeya wakiwemo wataalamu wa ujenzi,
polisi, usalama wa taifa na wataalam wa masuala ya fedha.
|
RC MAKALA ATEUA KAMATI YA KUCHUNGUZA MRADI WA BILIONI 4.8
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment