Kada wa Chama cha Mapinduzi, Steven Wasira amesema kuwa
wapinzani wamekosa hoja za kuongelea hivyo wamebaki kupiga kelele.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.
Amesema kuwa dhana ya kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa
hizo ni propaganda ambazo wamekuwa wakizieneza makusudi.
“Hawa jamani sasa hivi wanatapa tapa tu, wameishiwa hoja, ndio
maana kila siku wanakimbilia kwenye mitandao kutukana viongozi wa nchi,”amesema
Wasira
Kwa upande wake, Mustaph Muslim aliyehamia chama hicho akitokea
chama cha demokrasia na maendeleo, amemshauri Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu
Nchema kumshughulikia Mange Kimambi anayeishi nchini Marekani.
WASIRA WAPINZANI WAMEBAKI KUPIGA KELELE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment