Katibu mkuu wa Wizara ya mifugo
Dkt.Mary Mashingo amesema Serikali haina mpango wa kuongeza muda wa zoezi la
upigaji chapa kwa ng'ombe wala punda na kuwataka wenye mifugo hiyo
kuhakikisha wanafanya hilo ndani ya muda uliowekwa.
Katibu mkuu huyo amesema mpaka
sasa ng'ombe milioni kumi na tatu laki
tano ,elfu hamsini na moja na hamsini na moja sawa na asilimia 77.9 ya
ngo'mbe waliotarajiwa kupigwa chapa tayari wamepigwa chapa
|
Kwa upande wa punda,Dr.Mashingo
amesema mpaka sasa punda elfu moja mia
moja na sabini na nne wamepigwa chapa kati ya punda laki tano ,sabini na
mbili elfu mia tatu hamsini na tatu
|
Mpaka sasa Wilaya ya Mafia iliyopo
mkoa wa Pwani ndiyo wilaya pekee ambayo haijaanza zoezi hilo la upigaji chapa
linalotarajiwa kufikia tamati tarehe 31 ya mwezi huu
|
Serikali imesema haina mpango wa kuongeza muda wa zoezi la upigaji chapa kwa ng'ombe wala Punda.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment