Halmashauri ya mji wa Mbinga
mkoani Ruvuma imewafukuza kazi watumishi wake 58 kwa makosa mbalimbali
ikiwemo kughushi vyeti vya kidato cha nne na wengine kwa kuisababishia hasara
halmashauri hiyo.
|
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa
Mbinga Mheshimiwa Egno Kipwere ambapo watumishi waliofukuzwa kazi ni wa kada
mbalimbali wakiwemo walimu na maofisa watendaji pamoja na afisa misitu wa
halmashauri hiyo Bw. David Hyera ambaye amefukuzwa kazi kwa kuisababishia
hasara halmashauri hiyo kwa kuuza mbao na miti katika msitu wa Mbambi
|
WATUMISHI 58 WAFUKUZWA KAZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment