Waziri wa Viwanda
Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amekiri ni kweli serikali ya
Tanzania inadaiwa na viwanda vya ndani huku akidai wanaosababisha deni
lisilipwe ni watanzania wasiolipa kodi.
Waziri Mwijage amebainisha hayo leo
(Jumatano) katika mkutano wa Bunge wa 10 kikao cha Pili kinachoendelea
kufanyika mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza kwenye wizara yake
ambapo aliulizwa kwamba serikali ina mkakati gani madhubuti wa kulipa madeni
hayo ili kuweza kunusuru anguko la viwanda ambavyo vimeanzishwa kwa nia njema.
"Kwa niaba ya serikali nasema
ndio serikali inadaiwa na sasa tunaongeza jitihada za kuhakikisha kwamba kila
stahili ya serikali inakusanywa na kile kitakachokusanywa ndicho
tutakachowalipa wale", alisema
Waziri Mwijage.
Pamoja na hayo Waziri Mwijage
aliendelea kwa
kusema "hatujawalipa
wale kwa sababu nasi hatujalipwa, kuna watu hawapendi kulipa kodi na Tanzania
tunafanya vibaya kwa sababu kuna watu hawataki kulipa kodi lakini katika nchi
nyingine huwezi kupewa haki nyingine hata kuchumbia kama huwezi kuonyesha 'tax
clearance'".
WAZIRI MWIJAGE "NI KWELI SERIKALI INADAIWA "
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment