Rais Dkt. John Magufuli
amesema kuzinduliwa kwa hati ya kusafiria Kielektroniki, nchini Tanzania
itaweza kusaidia kupunguza usumbufu kwa watanzania pindi wanapotaka kwenda nje
ya nchi.
Rais Magufuli ameeleza hayo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa hati hiyo ambapo amesema kuwa huo ni
mwanzo wa utekelezaji mkubwa wa uhamiaji mtandao ambao umepangwa kutekelezwa
kwa awamu nne ili kuboresha zaidi utoaji wa vibali mbalimbali vinavyotolewa na
uhamiaji.
"Passport tunayoizindua leo ina
alama nyingi za usalama, hii itasaidia kupunguza, kama si kuondoa kabisa
uwezekano wa kughushiwa. Zaidi ya hapo baadhi ya taarifa zake zitakuwa
zinasomeka kwenye mifumo ya kielektroniki bila kulazimika kuipeleka
yenyewe", alisema Dkt
Magufuli.
Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli
amesema mara baada ya awamu hiyo awamu ya pili itakua ni kufunga mfumo wa viza
ya kielektroniki pamoja na hati za ukaaji za kielektroniki ambapo awamu ya tatu
itakua ni usimamizi wa mipaka kwa njia za kielektroniki pamoja na kupanua
huduma nyingine.
RAISI JPM"PASSPOT ZITAPUNGUZA USUMBUFU"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 31, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment